Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Suala la ukosefu wa ajira kwa vijana lapata muarobaini Tanzania

Suala la ukosefu wa ajira kwa vijana lapata muarobaini Tanzania

Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa uchumi wa Tanzania umekua kwa asilimia 7 lakini licha ya mafanikio haya, ukosefu wa ajira miongoi mwa vijana bado ni changamoto kubwa ikiwa katika kiwango cha asilimia 12.

Yaelezwa kuwa kwa kila vijana 700,000 ambao wanasaka ajira kila mwaka ni fursa 40,000 tu ambazo ziko wazi hii ikimaanisha kwamba ni asilimia 6 tu ya vijana ambao wanapata kazi rasmi. Hali hiyo imesababisha Umoja wa Matifa kupitia shirika lake la maendeleo ya viwanda, UNIDO, kuanza mipango rasmi ili kukabiliana na changamoto hizo. Kufahamu ni hatua gani Umoja wa Mataifa umechukua ungana na Grace Kaneiya katika makala hii.