Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maisha ughaibuni si lelemama, yapaswa kujituma na kufanya bidii: Mhamiaji kutoka Tanzania

Maisha ughaibuni si lelemama, yapaswa kujituma na kufanya bidii: Mhamiaji kutoka Tanzania

Ikiwa Disemba 18 ni siku ya wahamiaji duniani, Umoja wa mataifa unataka mazingira bora yawekwe kwa mamilioni ya watu ambao wanahama makwao na kwenda nchi za ugenini kwa sababu zinazotofautiana ikiwemo katika juhudi za kuimarisha maisha yao.

Kuna zaidi ya watu milioni 232 waliohama makwao ulimwenguni. Wahamiaji wanapoondoka nchi zao za kuzaliwa wanakumbana na mazingira mapya ambayo ni tofauti na yale waliozoea. Haji Hamis ni mkaazi wa Marekani ambaye alitoka Tanzania miaka 13 iliyopita ili aweze kujitafutia maisha bora katika Mahojiano maalum na Joseph Msami wa idhaa hii ameelezea yale anayokumbana nayo akianza kwa kulinganisha hali ilivyokuwa enzi hizo na hivi sasa.

(MAHOJIANO YA JOSEPH NA HAJI)