Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mshikamano wa kibinadamu utatue changamoto za jamii-Ban

Mshikamano wa kibinadamu utatue changamoto za jamii-Ban

Ukosefu wa usawa , ufukara na ukosefu wa ajira ni miongoni mwa mambo yanayohitaji mshikamno katika kuyatatua, amesema Katibu Mkuu Ban Ki-moon katika ujumbe wake kwa siku ya kimataifa ya mshikamano wa kibinadamu hii leo.

Ban amesema licha ya mafaniko ya maendeleo ya kibinadamu kwa miongo miwili iliyopita, changamoto hizo zinapaswa kutatuliwa kwa mshikamano ili kuziba pengo katika kuhakikisha maendeleo endelveu.

Kadhalika ametaja changamoto nyingine kuwa ni ubaguzi unaoendelea kuwa kikwazo katika ujenzi wa jamii jumuishi, pamoja na mabadiliko ya tabianchi yanayotajwa kuathiri zaidi wale ambao hawakuyachangai kwa kiwango kikubwa.

Katibu Mkuu ametaka msisitizo wa jukumu la mshikamano wa kibinadamu katika kujenga maisha ya utu kwa wote katika sayari dunia.