Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baridi kali tishio jipya kwa watoto mashariki ya kati

Baridi kali tishio jipya kwa watoto mashariki ya kati

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF limesema msimu wa baridi kali isiyo ya kawaida unanyemelea mashariki ya kati na kuweka mamilioni ya watoto walioasambaratishwa na vita katika hali mbaya zaidi.

UNICEF inasema watoto wenye utapiamlo na udhaifu kutokana na ukosefu wa huduma za afya katika kambi na makazi ya muda wamo hatarini zaidi kupatwa na hali ya mwili kutoweza kustahmili baridi kali vile vile magonjwa ya kupumua.

Hivyo shirika hilo linatarajia kufikia watoto milioni 2.5 nchini Syria, Iraq, Jordan, Lebanon,Uturuki na Misri, kutoa huduma za nguo na blanketi za joto, msaada wa kifedha kwa familia pamoja na huduma zingine, operesheni ambayo UNICEF inasema itasababisha pengo la dola milioni 38 katika mfuko wake.