Kijiji kilichoko ziwani chapata nuru kwenye huduma za afya ya uzazi

Kijiji kilichoko ziwani chapata nuru kwenye huduma za afya ya uzazi

Afya ya uzazi moja ya vipengele vya lengo namba tatu la malengo endelevu, SDGs linalotaka hakikisho la afya na ustawi wa watu wote ikiwemo wanawake na wasichana. Nchini Benin hasa kwenye eneo la kusini la f Sô-Ava hali inatia shaka na shuku kwa kuwa eneo hilo liko ziwani na makazi yamezingirwa na maji na hivyo kusababisha huduma za afya ya uzazi wa mpango kukumbwa na changamoto.

Wanawake wanabeba ujauzito hata kama hawana ridhaa, halikadhalikawasichana. Je hali ikoje na nini kinafanyika? Ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii.