Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kilio cha raia wa Aleppo kisikiwe: Zeid

Kilio cha raia wa Aleppo kisikiwe: Zeid

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu katika Umjoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein ametaka jumuiya ya kimataifa kukisikia kilio cha wanawake, wanaume na watoto ambao wanatshwa na kuchinjwa mjini Allepo nchini Syria,na kuchukua hatua za haraka za kuwakomboa.

Ofisi ya haki za bianadmu OHCHR, imepokea taarifa za uhakika za kuuawa kwa raia kwa makombora, au mauaji ya kiholela yanayotekelezwa na vikosi vya serikali, huku miili ikizagaa mitaani mashariki mwa Allepo. Hata hivyo wakazi wa maeneo hayo wanashindwa kuzihudumia maiti hizo kutokana na mfululizo wa makombora na hofu ya kulipuliwa.

Kadhalika taarifa hizo zinadai kuwa vikosi vya serikali na washirika wake, vimeripotiwa kuingia majumbani kwa raia na kuwaua watu ambapo jana pekee watu 82 wameuawa, 11 miongoni mwao wakiwa ni wanawake na watoto 11.

Rupeet Colville ni msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu.

( Sauti ya Colville)

‘‘Serikali ya Syria ina jukumu la kuheshimu na kulinda haki ya maisha ya raia pamoja na wapiganaji ambao wamejisalimisha na kuweka chini silaha zao.’’