Wimbi refu zaidi larekodiwa bahari ya Atlantic: WMO

13 Disemba 2016

Kamati ya wataalamu wa shirika la kimataifa la utabiri wa hali ya hewa WMO , wamebaini rekodi mpya ya wimbi refu kuwahi kurekodiwa duniani likiwa na mita 19 au futi 62.3 ya vipimo vya buoy huko Atlantic Kaskazini.

Kwa mujibu wa shirika hilo wimbi hilo limerekodiwa tarehe 4 Fenruary 2013 katika bahari ya Atlantic Kaskazini kati ya taifa la Iceland na uingereza . Wimbi hilo limetokana na kuvuma kwa upepo mkali katika eneo hilo la bahari.

Rekodi iliyovunjwa ambayo imekuwa ndio ya juu kwa muda mrefu ni mita 18.275 au futi 59.96 iliyorekodiwa 8Desemba 2007. Claire Nullis ni msemaji wa WMO.

(SAUTI YA CLAIRE NULLIS)

“sio tu kutangaza rekodi nyingine mpya ya dunia , inatusaidia kupata taswira kamili ya mawimbi ya kupindukia katika bahari ya atlantic ambayo tunahitaji kuyafahamu hasa kwa kuhakikisha usalama wa usafiri wa majini.”

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter