Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushindi wa mgombea asiyestahili watia hofu HirShabelle Somalia

Ushindi wa mgombea asiyestahili watia hofu HirShabelle Somalia

Umoja wa Mataifa, Muungano wa Ulaya, Muungano wa Afrika, IGAD, serikali za Ethipia, Sweeden, Italia , Uingereza na Marekani wamesema wanahofia uendeshaji wa uchaguzi wa wa Jumapili wa bunge dogo au bunge la wananchi kwenye mji wa HirShabelle mkoa wa Jowhar ambapo mshindi amekuwa ni mgombea asiyestahili.

Hivi karibuni timu ya usimamizi wa uchaguzi nchini Somalia (FIEIT) ilisema mgombea huyo Mheshimiwa Mohamed Abdullahi Hassan, anayemaliza muda wake katika serikali ya shirikisho kama waziri wa Vijana na michezo,hastahili, pamoja na mgombea mwingine Ahmed Sheikh Nur, kwa kuhusika kwao katika ghasia ambazo zilitokea ndani na nje ya kituo cha kupigia kura mkoani Jowhar mwezi uliopita ,watu kadhaa, ikiwa ni pamoja na wajumbe wa uchaguzi, walijeruhiwa.

Jumuiya ya kimataifa inasema kufanyika kwa uchaguzi huo jana Jowhar ni kupuuza barua iliyotumwa na timu ya usimamizi wa uchaguzi Disemba 7 kwa timu ya HirShabelle na Rais Ali Abdullahi Osoble ikieleza bayana kumpiga marufuku ya kugombea kiti cha ubunge bwana Hassan na bwana Nur . kiti hicho kimetengewa ukoo wa Jidle clan.