Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres ala kiapo; atangaza hatua kurejesha imani kwa UM

Guterres ala kiapo; atangaza hatua kurejesha imani kwa UM

Antonio Guterres kutoka Ureno ameapishwa leo kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, mbele ya wawakilishi wa nchi 193 wanachama wa Umoja huo. Assumpta Massoi na ripoti kamili.

(Taarifa ya Assumpta)

Ndani ya ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Rais wa Baraza Kuu, Peter Thomson akiitisha kikao mahsusi kwa ajili ya kuapa kwa katibu Mkuu wa Tisa, Antonio Guterres.

image
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akihutubia Baraza Kuu baada ya azimio kuhusu mchango wake kupitishwa kwa kauli moja. (Picha:UN/Evan Schneider)
Mwakilishi wa kundi la Asia na Pasifiki, akawasilisha azimio namba… mahsusi la kuchaguliwa rasmi kwa Guterres …ambapo Bwana Thomson akauliza wajumbe wa Baraza iwapo wanaridhia au la..

Hatua hii ilifuatiwa na matamko kutoka kanda mbali mbali zinazowakilishwa kwenye Umoja wa Mataifa na hatimaye kiapo..

 “Mimi, António Guterres, naapa kutekeleza majukumu yangu kwa uaminifu, utashi na uelewa wa majukumu ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, kutekeleza majukumu haya na kuzingatia mwenendo wangu kwa maslahi ya Umoja wa Mataifa na kwa mtazamo ambamo kwao si kwa kusaka au kukubali maelekezo ya utendaji wangu kutoka serikali au mamlaka yoyote nje ya chombo hiki.”

Baada ya kiapo Katibu Mkuu huyo anayeanza rasmi majukumu yake tarehe Mosi mwezi ujao akahutubia akisema dunia ya sasa inakabiliwa na changamoto kubwa, ikiwemo mgawanyiko kati ya wananchi na serikali,wananchi wakizikataa serikali akisema..

(Sauti ya Guterres)

“Wengi wamepoteza imani siyo tu na seriklai zao bali pia na taasisi za kimataifa ikiwemo Umoja wa Mataifa.”

Katibu Mkuu mteule akaenda mbali zaidi akisema Umoja wa Mataifa ulizaliwa baada ya vita na hivyo kazi yake sasa ni kuendeleza amani huku maendeleo yakiwa ni kitovu cha kazi yake. Hata hivyo amesema..

(Sauti ya Guterres)

“Umoja wa Mataifa unapaswa kuwa elekevu, ufanye kwazi kwa tija na kwa uhodari. Ujikite kwenye kutoa huduma bila michakato mirefu, uhudumie watu wengi bila urasimu. Haitoshi tu kufanya kazi kwa ubora, bali pia tuwe na uwezo wa kutangaza vyema kile tunachofanywa kwa njia ambayo kila mtu ataelewa.”

Hivyo amesema ni wakati wa kujenga upya uhusiano kati ya wananchi na viongozi wao kitaifa na kimataifa na kwa mantiki hiyo ametaja vipaumbele vyake vitatu atakavyozingatia..

 (Sauti ya Guterres)

“Nataka kuangazia vipaumbele vitatu vya kimkakati kwa ajili ya mabadiliko. Kazi yetu ya kuleta amani, usaidizi wetu kwa maendeleo endelevu na usimamizi wetu wa ndani.”

Guterres ingawa ameapa leo, ataanza rasmi majukumu yake tarehe Mosi Januari mwakani baada ya Katibu Mkuu wa sasa Ban Ki-moon kuhitimisha jukumu lake la miaka kumi tarehe 31 mwezi huu.