Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kongamano kuhusu usimamizi wa mtandao laendelea Mexico

Kongamano kuhusu usimamizi wa mtandao laendelea Mexico

Takribani watu bilioni nne kote duniani hawana fursa ya mtandao wa intaneti. Flora Nducha na ripoti kamili.

(Taarifa ya Flora)

Hayo yameelezwa kwenye kongamano la tisa la kimataifa kuhusu utawala wa mtandao linaloendelea huko Mexico likijadili njia za kutoa fursa ya mtandao wa intaneti duniani hasa katika nchi masikini.

Teknolojia ya habari na mawasiliano (ICT) ni nyenzo muhimu katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu kwa mujibu wa msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi Lenni Montiel, akisema...

(SAUTI YA LENNI)

" Teknolojia hususani intaneti ni jukumu kubwa katika elimu, kuboresha maisha ya watu wenye ulemavu, huduma za afya katika katika Nyanja zote za maisha, na hasa tunazozungumzia suala la kutolipuuzia”

Kongamano hilo limewaleta pamoja washiriki zaidi ya 3000 wakiwakilisha serikali, sekta binafsi na wataalamu wa ICT.

Watajadili pia masuala ya haki za binadamu, uhuru wa kuongea, usalama wa mtandao na ushirikino wa kimataifa katika maendeleo ya intaneti.