Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chekechea kazini zakuza ajira Jordan: ILO

Chekechea kazini zakuza ajira Jordan: ILO

Uwepo wa shule za awali maarufu kama chekechea katika maeneo ya kazi, nchini Jordan, zimesaidia akina mama kukabiliana na changamoto ambazo huwazuia wengi wao kuingia katika soko la ajira.

Shirika la kazi dunini ILO linapigia chepuo hatua hiyo likisema inakuza ajira kwa kuongeza uzalishaji. Sheria ya kazi Jordan, inayataka kampuni zilizoajiri wanawake zaidi ya 10 na wenye watoto walio chini ya miaka minne kuanzisha chekechea sehemu za kazi.

Suhair Shwairah mama wa mtotmo Mohamed mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu na anyefanya kazi katika kiwanda cha nguo mjini Madaba, huenda na mwanaee kazini kila siku na kukabidhi kwa walimu. Akiwa mwenye furaha anasema.

(SAUTI SUAHIR)

‘‘Chekechea imebadili maisha yetu, kwa sababu hakuna mtu aliyekuwa anamhudumia mwanangu awali, sasa tunajisikia salama sana, Mohammad ana furaha sana awapo chekechea’’