Takwimu za satelaiti ni muhimu kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
Takwimu zinazokusanywa kwa njia ya satelaiti ni muhimu katika harakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Hayo yamesemwa na Dr. Ali Omar, afisa katika shirika la Marekani linalohusika na masuala ya sayansi na teknolojia ya anga na hali ya hewa NASA, katika idara ya serikali, kitengo cha mabadiliko ya tabianchi. Anahudhuria mkutano wa mabadiliko ya tabianchi au COP22 mjini Marakech Morocco.
Amesema NASA ambayo imekuwa ikikusanya takwimu za nchi mbalimbali kwa miaka mingi imeziwasilisha kwenye mkutano wa COP22 na kuzitoa bure sababu..
(SAUTI DR OMAR 1)
Amesema maendeleo na ongezeko la gesi ya ukaa vinachangia mabadiliko ya tabianchi ambayo yanaathari kubwa akitolea mfano Afrika kwenye jangwa la Sahara..
(DR OMAR 2)