Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dola milioni 12 zatengwa kwa ajili ya mahitaji ya dharura ya kibinadamu CAR

Dola milioni 12 zatengwa kwa ajili ya mahitaji ya dharura ya kibinadamu CAR

Chini ya mamlaaka ya mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa mataifa (OCHA) nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, Fabrizio Hochschild, mfuko wa masuala ya kibinadamu nchini humo (HF CAR) umeidhinisha ufadhili wa miradi 26 kwa gharama za dola milioni 12 .

Miradi hiyo itaendeshwa na mashirika yasiyo ya kiserikali NGO’s ya kitaifa na kimataifa na mashirika ya Umoja wa Mataifa.

OCHA inasema fungu hilo la fedha,limewasili katika wakati muafaka ambapo kuna ongezeko kubwa la maeneo yanayohitaji msaada na kuendelea kwa machafuko CAR, hali ambayo imeongeza mahitaji mapya ya kibinadamu ambayo awali hayakuwa na ufadhili au fuku kutoka mpango wa kmisaada ya kibinadamu kwa mwaka 2016.

Miradi itakayofadhiliwa na fedha hizo ni mahitaji ya kiafya, vita dhidi ya utapia mlo, elimu, maji safi na usafi, ulinzi na msaada wa kurejesha fursa za masuala ya kibinadamu.

Miradi hiyo itasaidia mahitaji ya maelfu ya wakimbizi wa ndani, jamii zinazowahifadhi na kusaidia hatua ya awali ya kurejea nyumbani kwa wakimbizi wa ndani.

Hadi leo hii ni theluthi ombi la dola milioni 532 zinazohitajika kwa masuala ya kibinadamu CAR limefadhiliwa kwa theluthi tu.