Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

G2O waanzisha sera za kuwezesha uwekezaji wa nje- UNCTAD

G2O waanzisha sera za kuwezesha uwekezaji wa nje- UNCTAD

Nchi tisa wanachama wa G-20 wameanzisha hatua za kisera kufuatilia uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje ambao umetajwa kuwa ni muhimu katika kufufua uchumi wa dunia, imesema Kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa mataifa, UNCTAD.

Kwa mujibu wa ripoti mpya ya UNCTAD, nchi kama vile Argentina, India na Saudi Arabia zimechukua hatua katika sekta kadhaa huku Marekani na China zikipitia mahitaji ya wawekezaji wa nje.

Ripoti hiyo pia inasema Japan, Canada na Uturuki nazo zimekamilisha mikataba ya kimataifa ya uwekezaji (BTs) huku jumuiya ya Ulaya nayo ikikamilisha mkataba wake wa uwekezaji na jumuiya ya uchumi ya kusini mwa Afrika SADC.

UNCTAD katika ripoti hiyo inasisitiza kuwa iwapo kundi la G20 litalinda ahadi yake ya kujenga uchumi ulio wazi, na kuwezesha uwekezaji wa kimataifa watathimini ikiwa vikwazo vilivyopo katika uwekezaji wa nje vyaweza kupunguzwa.