Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tume ya kurejesha wakimbizi Burundi ni tumaini jipya: Mbilinyi

Tume ya kurejesha wakimbizi Burundi ni tumaini jipya: Mbilinyi

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR nchini Burundi linasema suala la urejeshwaji wa hiari kwa wakimbizi wa nchi hiyo linatarajiwa kupatiwa msukumo baada ya kuundwa kwa tume mpya itakayoratibu mchakato huo.

Mwakilishi mkazi wa UNHCR Burundi Abel Mbilinyi, ameiambia idhaa hii katika mahojiano kuwa, tume hiyo tarajiwa inatokana na ushauri wa Msaidizi wa

Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Volker Turk aliyefanya ziara nchini Burundi juma moja lililopita.

( SAUTI MBILINYI)

Kadhalika Mbilinyi anaeleza namna tume hiyo itakavyoepuka mambo ya kisiasa na kujikita katika utendaji.

( SAUTI MBILINYI)