Mashirika ya kiraia wajibisheni serikali- Ban
Hatimaye mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi umeanza kutekelezwa leo tarehe 4 ya mwezi Novemba ambapo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu Ban Ki-moon amekuwa na mkutano na wakilishi wa mashirika ya kiraia. Amina Hassan na ripoti kamili.
(Taarifa ya Amina)
Mkutano ulihusisha wawakilishi wa mashirika ya kiraia hata walio mbali kuzungumzia wanachofanya kufanikisha mkataba wa PAris unataoka kupunguza kiwango cha joto duniani. Huyu ni mmoja wao kutoka Guatemala akigusia mradi ambao kwao mtoto anahuisha taka ili kuzalisha bidhaa mpya.
Ban katika hotuba yake akasema mashirika ya kiraia yamekuwa mstari wa mbele na ndio maana ameamua kutumia siku hii ya kihistoria kukutana nao na kuwasikiliza kwa kuzingatia mchango wao katika kufanikisha kupitishwa kwa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi.
Hata hivyo amesema ..
“Bado tunakimbizana na muda. Tunahitaji kuanza kuelekea kwenye mustakhbali wa kiwango kidogo cha uchafuzi na wa kukabiliana na tabianachi. Kwa hiyo nawasihi kuendelea na mapambano. Wajibisheni serikali na msisitize kuchukuliwa kwa hatua.”