Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kujitioa ICC sio sahihi: Ban

Kujitioa ICC sio sahihi: Ban

Tamko la nchi tatu za Afrika la kujitoa kwenye mkataba wa mahakama ya kimataifaya uhalifu ICC, linatuma ujumbe mbaya amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

Akiongea na wajumbe wa baraza la usalama Ijumaa, Ban amesema kujitoa kwa Afrika Kusini, Gambia na Burundi kwa uanachama kunaathiri majukumu ya uketekezaji wa haki.

Amesema kupitia mahakama hiyo dunia imepiga hatua kubwa katika mfumo wa sheria ambayo imetoa usalama dhidi ya uhalifu bila kuchukuliwa hatua.

Hata hivyo Katibu Mkuu Ban amekiri kuwa, sio nchi zote ambazo zilikubali mamlaka ya ICC, na kwamba hadi sasa ni waafrika pekee ndiyowaliopatikana na hatia licha ya ushahidi wa uhalifu, mauaji ya kimbari, uhalifu wa kivita dhidi ya binadamu kila mahali.

Ameongeza kuwa licha ya hayo, kujitoa kwa nchi tatu ni kosa.

( SAUTI BAN)

‘‘ Najutia hatua hizi, ambazo huenda zikatumaa ujumbe mbaya kwa nchi hizi katika uwajibikaji wake kwenye sheria. Changamoto hizi zaweza kushughulikiwa sio kwa kuondoa usaidizi kwa mahakama lakini kuiimarisha ukiwa ndani yake.’’