Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ugaidi ni “zimwi” lisilo na mpaka: Pakistani

Ugaidi ni “zimwi” lisilo na mpaka: Pakistani

Mikakati ya kimataifa ndio njia pekee ya kupambana na ugaidi, na hiyo ni kauli ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistani, Hina Rabbani Khar aliyoitoa mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumane wakati wa mjadala wa wazi kuhusu vita dhidi ya ugaidi.

Bi.Khar ambaye aliendesha mjadala huo kwa kuzingatia Pakistani ndio Rais wa sasa wa Baraza hilo, amesema ugaidi unaendelea kuwa tishio kwa kila nchi kwa hiyo jitihada za pamoja zinahitajika kukabiliana nao.

(SAUTI YA HINA)

“Muongo uliopita umedhihirisha kuwa ugaidi hautambui mpaka. Katika muongo huo  somo ambalo sote tumejifunza ni kwamba mkakati wa nchi moja hauwezi kufanya kazi kudhibiti ugaidi ambao ni sawa na zimwi, zimwi ambalo lina tentacles dunia nzima. Hii ni dhahiri kitisho cha dunia hivyo basi mipango ya kukabiliana nalo ni lazima iwe na sura ya kimataifa.”

Halikadhalika Bi. Khar amesema ugaidi na msimamo mkali kuhusu jambo fulani haviwezi kuhusishwa na kamwe visihusishwe na dini, rangi au jamii yoyote ile duniani.