Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Fursa na usalama ni muhimu kwa usafiri endelevu

Fursa na usalama ni muhimu kwa usafiri endelevu

Sekta ya usafiri ina jukumu kubwa katika maendeleo ya nchi, kwa kuwezesha wafanyakazi kufika kazini na bidhaa kufika sokoni.

Licha ya umuhimu huo bado kuna changamoto kubwa kwa nchi na sekta nzima ya usafiri kutoa fursa yay a usafiri salama, wa gharama nafuu na wa kuaminika.

Hayo ni kwa mujibu wa wataalamu wa kimataifa walioteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa kutoa mapendekezo kwa ajili ya mifumo imara na bora zaidi kiafya.

José Viegas, ni mjumbe wa kundi hilo la usauri la ngazi ya juu kuhusu usafiri endelevu ambalo limetoa ripoti yake na kuiwasilisha kwa Kastibu Mkuu wa Umoja wa mataifa , anaeleza umuhimu wa sekta ya usafiri

(VIEGAS CUT 1)

“Usafiri ni muwezeshaji wa maendeleo, kupitia fursa inaytoa kwa watu na bidhaa, watu kwa kuwapeleka makazini, masokoni, maeneo ya umma, kwa huduma za jamii , kwa uhusiano wa kijamii na bidhaa kwenda masokoni. Kama huna fursa ya mifumo yote hii basi huna maendeleo”

Lakini ameongeza changamoto zipo

(VIEGAS CUT 2)

"Zipo nyingi, hasa katika kutenga maeneo kwa magari binafsi, watembea kwa miguu na waendesha baiskeli haipewi uzito kama magari. Hata kama hali ni mabya ya msongamano kwa magari basi ni mbaya zaidi kwa wanaotaka kutembea kwa miguu au kuendesha baiskeli au hata kutumia usafiri wa umma.”