Dansi, mavazi na nyimbo zatamalaki siku ya wafanyakazi wa UM
Wiki hii Umoja wa Mataifa umeadhimisha siku ya wafanya kazi wa Umoja huo. Wafanyi kazi katika sehemu mbali mbali kuliko ofisi za Umoja wa Mataifa wameadhimisha siku hii kwa njia mbali mbali. Hapa makao makuu wafanyakazi wamefanya hafla maalum kwa ajili ya kuenzi vipaji vya wafanyakazi wake, hafla ya mwisho kufanyika ilikuwa muongo mmoja uliopita na hivyo maadhimisho hayo yamekaribishwa huku wafanyakazi wakishiriki kwa njia mbali mbali ikiwemo kuvaa mavazi ya kitamaduni, kucheza dansi, kughani mashairi na pia kuimba. Bryan Lehander alikuwa shuhuda wetu na anatusimulia yaliyojiri katika makala hii.