Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vikundi vya kigaidi ISIL vyafukuza maelfu ya wananchi na kunyonga mamia ya watu: Mosul Iraq

Vikundi vya kigaidi ISIL vyafukuza maelfu ya wananchi na kunyonga mamia ya watu: Mosul Iraq

Ofisi yahakiza bunadmau ya Umoja wa Mataifa imelaani vitendo vinavyotekelezwa na kundi la kigaidi la ISIL kuwalazimisha mamia ya maelfu ya watu kuyakimbia makazi yao katika wilaya karibu na Mosul na raia wengine kulazimishwa kuhamia ndani ya mji wenyewe tangu mapambano ya kivita yalianza tarehe 17 Oktoba kurejesha udhibiti wa serikali ya Iraq.

OHRC katiak taarifa yake imesema kuwa imepata taarifa za uhakika kuhusu vitendo hivyo ambapo pia imeongeza kuwa watu wanaonakataa kuzingatia amri hiyo ikiwemo vikosi vya Usalama wa Iraq pamoja na raia 232 walipigwa risasi na kuuawa Jumatano iliyopita.

Inakisiwa takriban familia 5,370 wametekwa nyara na kikundi hicho kutoka wilaya ndogo ya Shura, ikiwemo familia nyingine 160 kutoka wilaya ya al-Qayyarah na nyingine ya watu 2,210 kutoka wilaya ndogo ya Nimrud katika eneo la al-Hamdaniya na watu wengine 150 kutoka Hamam al-alil inayosemekana kuwa ngome ya kikundi hicho tayari kuna watu wapatao 60,000 ambapo idadi ya awali ilikuwa watu 23,000 pekee.

Akilaani hatua hiyo, Kamishna mkuu wa haki za binadamu Zeid Ra’ad Al Hussein, amesema matumizi ya ngao ya binadamu ni marufuku chini ya sheria za kimataifa, na ukiukaji wa haki za binadamu. Ameisisitiza kuwa ni muhimu kwa jeshi la serikali na washirika wao kuheshima sheria za kimataifa za haki za binadamu.