Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto Calais wamo hatarini:UNICEF

Watoto Calais wamo hatarini:UNICEF

Shirika la Kuhudumia Watoto, UNICEF limesema limesikitishwa mno na matukio ya jana usiku ambapo watoto wakimbizi wamelazimika kulala nje kwenye baridi baada ya kambi yao kuteketezwa moto huko Calais, Ufaransa. Halikadhalika, UNICEF imeshtushwa pia na habari zingine za watoto kutosajiliwa na kupewa vitambulisho na hivyo kurudishwa na polisi kambini.

Shirika hilo pia limesema, serikali ya Ufaransa na Uingereza ziliahidi kuwalinda watoto wakati kambi za Calais zikibomolewa, na iwapo hali hii itaendelea, basi itahatarisha usalama wao zaidi, na kurahisisha watoto kutumbukia kwenye mikono ya walanguzi na wasifirishaji haramu.

UNICEF inatoa wito kwa serikali hizo mbili kuhakikisha watoto wanalindwa wakati shughuli hizo za usajili zikiendelea.