Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yapaza sauti mtumishi wake wa zamani asifungwe jela

UNICEF yapaza sauti mtumishi wake wa zamani asifungwe jela

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema limehuzunishwa sana na ripoti ya kwamba mfanyakazi wake wa zamani Baquer Namazi amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela nchini Iran.

Taarifa ya UNICEF imesema marafiki na wafanyakazi wenzake wamehuzunishwa na kuingiwa na wasi wasi kwa adhabu dhidi ya Bwana Namazi ambaye amekuwa anashikiliwa nchini Iran tangu tarehe 22 Februari mwaka huu.

Bwana Namazi sasa ana umri wa miaka miaka 80 na UNICEF na marafiki zake wana hofu kubwa juu ya afya yake na hivyo wanaomba aachiliwe huru kwa misingi ya kibinadamu.

Wakati akihudumu UNICEF Bwana Namazi alishikilia nyadhifa mbali mbali ikiwemo kuwa mwakilishi wake huko Somalia, Kenya na Misri.

UNICEF inasema alifanya kaZamazi bila kuchoka kwa ajili ya watoto kwenye maeneo magumu na kwamba anastahili kustaafu kwa amani.