Skip to main content

Wasichana wa Chibok waliochiliwa huru wasitengwe- UNICEF

Wasichana wa Chibok waliochiliwa huru wasitengwe- UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linashirikiana wahisani mbali mbali ili wasichana 21 wa Chibok walioachiliwa huru hivi karibuni na Boko Haram waweze kujumuika vyema katika jamii. Amina Hassan na ripoti kamili.

(Taarifa ya Amina)

Akizungumza na waandishi wa habari, mjini Geneva, Uswisi, msemaji wa UNICEF, Christophe Boulierac amesema wasichana hao wanaweza kukumbwa na kunyanyapaliwa na mateso.

Amesema zaidi ya hayo, watoto waliowapata kutokana na ukatili wa kingono wa Boko Haram, wanaweza kukumbwa na kukatiliwa, kutelekezwa au hata ghasia, hivyo amesema..

(Sauti ya Boulierac)

“Wasichana walioachiliwa huru wasisahaulike, wanahitaji msaada wa kutosha kujenga upya maisha yao. Wahisani wamewezesha mradi wa UNICEF wa kusaidia kujumuisha upya kwenye jamii zaidi ya wanawake na wasichana 750 waliokumbwa na ukatili wa kingono kutoka kwa Boko Haram.”