Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO kushirikiana na Tanzania kuboresha kilimo Kagera

FAO kushirikiana na Tanzania kuboresha kilimo Kagera

Shirika la chakula na kilimo duniani FAO, kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania limeanza mpango wa kitaalamu kuwezesha kilimo cha kisasa kufanyika mkoani Kagera, kwa ajili ya kuhakikisha uhakika wa chakula.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya chakula duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Kagera, Mwakilishi mkazi wa shirika hilo nchini Tanzania Fred Kafeero, amesema licha ya kukumbwa na tetemeko la ardhi hivi karibuni mkoa huo ni muhimu kwa uzalishaji wa kilimo.

( SAUTI KAFEERO)

Kwa upande wake Waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi wa Tanzania Charles Tizeba, amesema mpango huo umekuja wakati muafaka hasa kwa kuzingatia kuwa mkoa huo umeathiriwa na mabadiliko ya tabianchi.

( SAUTI TIZEBA)