Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lajadili madhila ya huduma za afya katika maeneo ya vita

Baraza la usalama lajadili madhila ya huduma za afya katika maeneo ya vita

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limekutana kujadili huduma za afya katika maeneo ya kivita ambapo wadau wa afya wanaohudumia majeruhi na wagonjwa katika maneo yenye machafuko wameshiriki katika mjadala huo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelieleza baraza hilo kuwa inasikitisha kuwa maeneo yenye vita kama Syria, wakazi wa maeneo hayo wametelekezwa na hata pande kinzani haziheshimu sheria za kivita akitolea mfano wa vifo vya makumi ya watu katika hospitali nchini Yemen mapema mwezi uliopita.

Akilihutubia baraza hilo Rais wa shirika la madaktari wasio na mipaka MSF Joanne Liu, amesema inasikitisha kwamba pande kinzani katika vita zinaendelea kufanya vitendo haramu vya kushambulia hospitali, kuuwa wagonjwa na wahudumu wa afya.

Kwa upande wake Rais wa kamati ya kimataifa ya shirika la msalaba mwekundu ICRC Peter Maurer ambaye amewasilisha hotuba yake kwa njia ya video kutoka Geneva Uswis, ameitaka jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua kadhaa ikiwamo.

( SAUTI PETER)

‘‘Nawataka kuhakikisha kuwa vitedno vya mashambulizi dhidi ya watoa huduma za afya ambavyo vinakiuka mkataba wa Genevea vinaadhibiwa vikali kama vile sheria za ndani za nchi. Tungependa kuona uimarishwaji wa uwezo wa uchunguzi ili kuwawajibisha watekelezaji.’’