Skip to main content

Ban na Muburi-Muita,wajadili amani na usalama wa Maziwa Makuu

Ban na Muburi-Muita,wajadili amani na usalama wa Maziwa Makuu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekuwa na mazungumzo na Bwana Zachary Muburi-Muita, Katibu mkuu wa mkutano wa kimataifa kuhusu ukanda wa Maziwa Makuu, (ICGLR).

Ban amempongeza bwana Muita kwa kuteuliwa kwake kushika wadhifa huo na kupongeza ICGLR kwa kubeba bendera ya juhudi za kuchagiza amani na usalama katika kanda hiyo.

Masuala mengine yaliyojadiliwa na wawili hao ni mchakato wa mazungumzo yanayoendelea na juhudi za kusambaratisha makundi ya yenye silaha Mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC.

Pia wamezungumzia njia ambazo Umoja wa mataifa na ICGLR watazitumia kuimarisha ushirikiano wao.