Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Imam na Mtawa waleta nuru kwa wakimbizi DRC

Imam na Mtawa waleta nuru kwa wakimbizi DRC

Kwa zaidi ya miaka mitatu sasa, mapigano nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, kati ya waasi wa balaka walio wakristo na waasi wa seleka ambao ni waislamu, yamesababisha karibu nusu milioni ya watu kukimbia makazi yao, na zaidi ya nusu milioni wengine kuishia kuwa wakimbizi wa ndani. Viongozi wawili wa kiislamu na kikristo, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, hawakujali tofauti ya dini pindi walipowapokea wakimbizi wa dini tofauti katika kijiji chao. Makala ya Brian Lehander inasimulia zaidi...