Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wajadili usugu wa dawa za kuuwa wadudu mashambani

UM wajadili usugu wa dawa za kuuwa wadudu mashambani

Mjadala wa ngazi ya juu wunafanyika leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kujadili mbinu za kukabiliana na changamoto ya kuenea kwa usugu wa dawa za kuua wadudu mashambani. Grace Kaneiya na taarifa zaidi

(TAARIFA YA GRACE)

Mjadala huo ulioandaliwa na shirika la afya duniani WHO unajumuisha pia mashirika mengine kama la chakula na kilimo FAO , la afya ya mifugo duniani OIE na wadau mbalimbali wanaohusika na afya ya binadamu , mimea na mifugo.

Akizungumza kabla ya kuanza kwa mjadala huo Bwana Juan Lubroth ambaye ni mkuu wa idara ya sayansi ya wanyama katika shirika la FAO amesema

(SAUTI YA JUAN)

“Matumizi mabaya ya dawa za kuua wadudu mashambani kuna hatari mbaya kwa dawa da binadamu na hata dawa za mifug na kilimo. Na kulijadili suala hili katika ngazi ya kikao cha Baraza kuu la Umoja wa Mataifa, inamaanisha hili ni zaidi ya tatizo la madawa, linaweza kuathiri zaidi uchumi na kuweza kurejesha afya nyuma katika karne ya 19 au 18.”