Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Unyanyasaji wa kijinsia bado ni changamoto kubwa vyuo vikuu duniani .

Unyanyasaji wa kijinsia bado ni changamoto kubwa vyuo vikuu duniani .

Kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachohusika na masuala ya wanawake (UN Women) kwenye kikao kinachoendelea cha 71 cha Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kimetoa ripoti yake ya

kwanza iliyoandaliwa na viongozi 10 wa vyuo vikuu duniani .

Kwenye kongomano hilo la 10x10x10 lijulikanalo kama "HeForShe" limehusisha viongozi 10 wa nchi, wakuu 10 wa makampuni makubwa, na viongozi 10 wa vyuo vikuu duniani.

Kongamano hilo lililoanzishwa mwaka wa 2015 linatilia mkazo wa kuwekwa ahadi madhubuti na kuanza mchakato wenye mwelekeo wa kufikia usawa wa kijinsia katika makampuni, madarasani na katika miji mikuu ya dunia.

Inasemekana kuwa mmoja kati ya wanawake watatu duniani kote amekabiliwa na aina ya unyanyasaji kimwili au kingono katika maisha yake. Na inataja kuwa waathirika wengi zaidi hubaki kimya kutokana na aibu, hatia, au hofu.

image
Ujumbe HeForShe.(Picha:UM/Devra Berkowitz)
Ripoti hiyo inaeleza kuwa zaidi ya nusu ya idadi ya watu duniani ni wa chini ya umri wa miaka 30 na kiwango cha wanaohitimu kinapanda na kuwa ni fursa ya kipekee kwa vyuo vikuu kuleta mabadiliko.

Ripoti hii inaonyesha kukosekana kwa usawa muhimu kwenye vyuo vikuu na hali hiyo inaweza kushughulikiwa kwa kuangazia mosi uwiano wa wanaume na wanawake kuwakilishwa katika vitivo vya vyuo vikuu; pili nyanja za utafiti kwa wanasichana kuchagua masomo yao ; na tatu idadi ya wanafunzi wa kike katika vyuo vikuu iliinganishwe na uwezo wao sawa na taaluma wanazochagua.

Akiongea kwenye uzinduzi wa ripoti hiyo, Bi Phumzile Mlambo-Ngcuka ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa UN Women anasema kuna matumaini makubwa kwa kila kizazi cha wanafunzi wa vyuo vikuu

wanaohitimu kulenga mipango ya kukabiliana na vikwazo vya sasa vya usawa wa kijinsia.

image
Emma Watson ambaye ni balozi mwema wa UN Women.(Picha:UM/Mark Garten)
Wengine walio ongea kwenye uzinduzi huo ni Emma Watson ambaye ni balozi mwema wa UN Women and mkurugenzi mtendaji

wa UNESCO, Irina Bokova. Baadhi ya vyuo vikuu vilivyojihusisha ni Oxford cha Uingereza, Georgetown cha Marekani, Witwatersrand cha Afrika Kusini na vinginevyo.