Hatma ya Syria isisalie mikononi mwa mtu mmoja- Ban
Mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa umeanza hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa ukileta pamoja viongozi wa nchi 193 wanachama wa umoja huo kutoka pande zote za dunia. Flora Nducha na ripoti kamili.
(Taarifa ya Flora)
Nats..
Rais wa Baraza Kuu Peter Thomson akitangaza kuwa kikao kitaanza kwa kusikia ripoti ya Katibu Mkuu Ban Ki-moon..
Nats.. up out
Ban katika ripoti yake akaangazia masuala kadhaa ikiwemo amani na usalama akigusia mzozo wa Syria, na kitendo cha msafara wa misaada ya kibinamu kushambuliwa jana na misaada kusitishwa Aleppo kikaibua kauli hii..
“Nawasihi nyote mwenye ushawishi kumaliza mapigano na mazungumzo yaanze. Mchakato wa siasa umechelewa sana. Baada ya ghasia zote hizi, mustakhbali wa Syria haupaswi kusalia mikononi mwa mtu mmoja.”
Rais Barack Obama wa Marekani akiwa ni wa tatu kuhutubia, ikiwa ni mara ya mwisho, akasema dunia iko katika mkanganyiko wa hali ya juu licha ya maendeleo yaliyopatikana..
Na hivyo naamini kwa sasa sote tunakabiliwa na kuchagua, tusonge mbele na mfumo bora wa ushirikiano au turudi nyuma kwenye dunia iliyogawanyika na hatimaye kubaguana kwa misingi ya rangi, dini na makabila. Nataka nipendekeze leo kuwa ni lazima tusonge mbele na tusirudi nyuma.”