Ukimbizi huchagui kama kwenda mapumzikoni- Kapaya

Ukimbizi huchagui kama kwenda mapumzikoni- Kapaya

Jumuiya ya kimataifa ifahamu kuwa hizi si zama za kufungia milango wakimbizi, na badala yake iige mfano wa Tanzania katika kuwapatia hifadhi ya kudumu wakimbizi.

Hiyo ni kwa mujibu wa mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR nchini Tanzania, Chansa Kapaya alipozungumza na Idhaa hii kuhuhu kile anachotaka kuona nchi zinaridhia kwenye mkutano wa leo wa wakimbizi na wahamiaji, akitaja hatua ya Tanzania ya mwaka 2010 ya kuridhia ombi la uraia kwa wakimbizi zaidi ya 200,000 wa Burundi

(Sauti ya Chansa)

“Huu ulikuwa uamuzi wa mwisho na wa kudumu kwa wakimbizi, na sasa tuko kwenye mchakato wa kuwapatia uraia.”

Bi. Kapaya amesema viongozi hao wachukua hatua za kijasiri akisema..

(Sauti ya Chansa)

“Kukimbia nyumbani kwa sababu ya vita, si kitu cha kuchagua kama unakwenda mapumziko, ni kwa sababu unaokoa maisha, unasaka usalama. Kwa hiyo kufunga milango hakutamsaidia mtu yeyote.”