Skip to main content

Ban azindua kampeni “kwa pamoja” kwa ajili ya wakimbizi na wahamiaji

Ban azindua kampeni “kwa pamoja” kwa ajili ya wakimbizi na wahamiaji

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezindua kampeni kwa ajili ya wakimbizi na wahamiaji iitwayo “Kwa Pamoja heshima usalama na utu kwa wote” , kampeni ambayo inapigiwa upatu kwenye mitandao ya kijamii.

Baada ya hotuba yake kwenye mjadala kuhusu wakimbizi na wahamiaji amesema Kampeni hiyo inalenga kutanabaisha mchango mkubwa wa wakimbizi na wahamiaji katika masuala ya uchumi, utamaduni na kijamii kwenye nchi watokako, wanakopitia na wanaokwenda kuweka makao mapya.

Ameongeza kuwa kampeni hiyo pia itasahihisha mtazamo potofu na taarifa zisizosahihio kuhusu wakimbizi na wahamiaji huku ikichagiza mawasiliano miongoni mwa wakimbizi na wahamiaji na wale walio katika nchi waendako.