Usalama wa wakimbizi ni muhimu kwenye vituo vya mapokezi:UNHCR
Hofu kubwa dhidi ya usalama wa waomba hifadhi nchini Ugiriki imeelezwa na Umoja wa Mataifa , baada ya kuzuka moto mkubwa kwenye kituo cha mapokezi kilichofurika umati wa watu.
Taarifa za awali zinaonyesha kuwa hakuna aliyepoteza maisha au kujeruhiwa vibaya katika ajali hiyo ya moto kwenye kituo cha Moria, kisiwani Lesvos, ambapo Shirika la Umoja wa M ataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, linasema ulianza baada ya kuibuka kwa ugomvi miongoni mwa wakazi.
Kwa mujibu wa William Spindler msemaji wa UNHCR, tukio hilo linathibitisha umuhimu wa usalama kwenye vituo vya mapokezi
Kuhama lazima iwe kitendo cha uchaguzi - FAO
Mkurugenzi Mkuu wa shirika la chakula na kilimo duniani FAO, José Graziano da Silva amesema hii leo kuwa kuhama kwa watu kutoka makwao kiwe kitendo cha kuchagua badala ya lazima.
Akizungumza kwenye kikao cha ngazi ya juu kuhusu wakimbizi na wahamiaji Bwana da Silva amesema ili hilo lifanikiwe ni vyema kuimarisha fursa za kuwaruhusu watu vijijini kuepuka kuhama makwao kutokana na shinikizo.
Kutambua mchango wa wakimbizi na wahamiaji ni muhimu sana-Somalia
Somalia inasema wakimbizi na wahamiaji wana mchango mkubwa katika jamii watokazo na waendako, tofauti na fikra za wengi kwamba watu hao ni chanzo cha madhila hasa kwa jamii zinazowapokea.
Hayo ni kwa mujibu wa mshauri wa kitaifa wa Somalia kuhusu masuala ya wakimbizi na wakimbizi wa ndani, Bwana Ahmed said Farah, aliyeiwakilisha nchi yake katika mjadala wa ngazi ya juu kuhusu wakimbizi na wahamiaji Jumatatu.
UNICEF na #GMG wapigia chepuo azimio la New York
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema kupitishwa kwa azimio la New York, kuhusu wakimbizi na wahamiaji ni hatua ya kwanza ya kushughulikia wimbi kubwa la hamahama ya watu ambayo dunia haijawahi kushuhudia.
Taarifa ya UNICEF imesema azimio hilo ambalo linaweka hatua za kimsingi za kuchukuliwa kulinda makundi hayo, litaokoa mamilioni ya watu wakiwemo watoto ambao wakati huu ni nusu ya wakimbizi duniani.