Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utumwa wa madeni wasalia kutesa wengi duniani- Ripoti

Utumwa wa madeni wasalia kutesa wengi duniani- Ripoti

Utumwa wa madeni umesalia mojawapo ya aina za utumwa wa zama za sasa ulimwenguni licha ya kupigwa marufuku kupitia sheria za kimataifa.

Ameonya leo mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa anayeangazia utumwa wa zama za sasa Urmila Bhoola wakati akiwasilisha ripoti yake mbele ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa.

Watu wapatao milioni 21 ni watumwa wakilazimika kufanya kazi ili kulipa madeni yao kwa kuwa hawana uwezo wa kulipa kwa njia nyingine.

Amesema umaskini, ukosefu wa njia mbadala za kiuchumi, ujinga na ubaguzi wa watu wa kimatabaka umesababisha watu kuchukua mikopo kwa malipo ambayo ni ajira zisizo na utu, ingawa ajira hiyo inazidi hata madeni wanayodaiwa.

Katika ripoti yake, Bi Bhoola ametaka kuelimisha umma kuhusu utumwa wa madeni na serikali zichukue hatua kuzingatia haki za binadamu na kutokomeza utumwa huo.