Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanaume huona aibu kwenda ngumbaru- Tanzania

Wanaume huona aibu kwenda ngumbaru- Tanzania

Nchini Tanzania ni asilimia 77 tu ya watu wazima na vijana ndio wanajua kusoma na kuandika hiyo ni kwa mujibu wa Baselina Levira, Mkurugenzi msaidizi, Elimu ya watu wazima na elimu njia ya mfumo rasmi Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia alipohojiwa na Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania. Bi. Levira alitoa takwimu hizo wakati wa siku ya kisomo duniani ambapo alisema kiwango hicho ni cha chini ikilinganishwa na miaka ya themanini ambapo ni asilimia Tisa nukta Sita tu ya watanzania ndio walikuwa hawajui kusoma na kuandika. Sasa hatua zinachukuliwa kurejesha kiwango cha ujuzi wa kusoma na kuandika kupitia miradi mbali mbali kama anavyoanza na mradi wa NAWEZA.