Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mikataba ya biashara itilie manaani haki za binadamu:De Zayas

Mikataba ya biashara itilie manaani haki za binadamu:De Zayas

Mikataba yote ya biashara ni lazima ifanyike kwa kuzingatia mikataba ya haki za binadamu , pamoja na malengo ya afya na mazingira , limeelezwa baraza la haki za binadamu.

Katika ripoti yake kwenye baraza hilo mjini Geneva, mtaalamu huru wa Umoja wa mataifa kuhusu haki za binadamu Alfred de Zayas makampuni makubwa ya biashara kwa kuanzisha sheria mpya ili kukidhi haja zao, ambazo amesema zinautenga umma.

Bwana de Zayas amesisitiza kwamba mikataba hii ya biashara inaathiri uwezo wa nchi kufuatilia makampuni ya kimataifa.

Ameongeza kuwa moja ya suluhu inaweza kuwa ni kujumuisha masuala ya haki za binadamu katika mikataba yote ya biashara, ikiwa ni pamoja na ile inayosimamiwa na shirika la kimataifa la biashara WTO.

Amesema wakati asasi za kiraia, jumuiya na makundi ya wanaharakati yatakuwa na jukumu kubwa katika mikataba ijayo ya biashara , wajibu wa kuingiza haki za binadamu katika mikataba hiyo utakuwa ni wa serikali, bunge na mahakama pia.