Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maeneo ya urithi yanaweza kuchangia makabiliano athari za mabadiliko ya tabianchi-UNESCO

Maeneo ya urithi yanaweza kuchangia makabiliano athari za mabadiliko ya tabianchi-UNESCO

Zaidi ya maeneo 1,800 kote duniani yaliyoteuliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO – kuwa katika urithi wa dunia yana jukumu muhimu katika kuelewa, kurekebisha na kukabiliana na athari mabadiliko ya tabia za nchi.

Ujumbe huu umetolewa  kwenye ufunguzi wa mjadala wa pili wa Huangshani, ambalo ni jukwaa la kimataifa katika maeneo ya yalioteuliwa na UNESCO na kuangazia maendeleo endelevu, na jukwaa limeandaliwa UNESCO na kituo cha elimu ya sayansi cha Uchina

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova kwa katika ujumbe wake wa video amesisitiza umuhimu wa mjadala huo akiutaja kama mchango kuelekea ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu (SDGs), kama pia mkakati mpya wa utekelezaji wa UNESCO.