Skip to main content

Tume maalumu ya uchunguzi imewasili Juba kufanyi kazi matukio ya Julai

Tume maalumu ya uchunguzi imewasili Juba kufanyi kazi matukio ya Julai

Tume huru maalumu ya uchunguzi , iliyotangazwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Agosti 23, kutathimini ghasia zilizozuka Juba kati ya Juali 8-25 mwaka huu, na pia jinsi mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS, ulivyochukua hatua, imewasili leo nchini Sudan Kusini kuanza kazi.

Timu hiyo inayoongozwa na Meja jenerali mstaafu Patrick Cammaert, itatathimini ripoti za matukio ya mashambulizi dhidi ya raia yaliyotokea ndani au katika maeneo ya jingo la Umoja wa Mataifa la ulinzi kwa raia Juba na kuamua endapo UNMISS ilichukua hatua zinazopaswa kuzuia na kukomesha mashambulizi hayo sanjari na kuwalinda raia kwa kutumia uwezo na rasilimali walizokuwa nazo wakati huo.

Pia timu hiyo itapaswa kutathimini hatua zilizochukuliwa dhidi ya shambulizi la kwenye hotel ya Terrain 11 Julai. Ghasia za Juali 2016 Juba zilisababisha vifo vya mamia ya watu na visa zaidi ya 217 vya unyanyasaji wa kingono na kijinsia kuorodheshwa, vikiwemo vitendo vya ubajaki wa watoto na wanawake katika maeneo mbalimbali ya Juba.

Timu hiyo inayojumuisha wataalamu wa jeshi, haki za binadamu, wataalamu wa masuala ya ukatili wa kingono na kijinsia, polisi na wanasheria inatarajiwa kuwasilisha ripoti yake kwa Katibu Mkuu ndani ya mwezi mmoja.