Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ronaldinho na udau wa Umoja wa Mataifa

Ronaldinho na udau wa Umoja wa Mataifa

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linatambua umuhimu wa kushirikisha ulimwengu wa michezo, kwani michezo ndio njia rahisi ya kupenya katika mioyo ya watoto na watu wazima duniani kote. Ushirikiano huu unasaidia UNICEF katika kupigia chepuo haki za watoto kucheza, kuwasilisha ujumbe maalum, kuhamasisha jamii na muhimu zaidi, kuhakikisha maendeleo endelevu ya watoto , familia na jamii. Moja ya timu inayoshirikiana na UNICEF ni FC Barcelona ya Hispani, na katika makala hii tunamulika ujumbe wao wakati wa ziara yao hapa kwenye Umoja wa Mataifa. Basi tuuangane na Amina Hassan.