Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wajumbe wa Baraza la Usalama wakutana na Rais Salva Kiir, Sudan Kusini

Wajumbe wa Baraza la Usalama wakutana na Rais Salva Kiir, Sudan Kusini

Wajumbe wa Baraza la Usalama wanakutana leo na Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir katika ziara yao ya siku tatu inayokamilika leo, kujadili maazimio yanayohusu Sudan Kusini yaliyopitishwa na baraza hilo.
Katika mkutano na Rais Salva Kiir, wajumbe hao wanatarajiwa pia kujadili jinsi Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNMISS utaendelea kufanya kazi na serikali ya Sudan Kusini katika kuboresha usalama na hali ya kibinadamu, ikiwa ni pamoja na majadiliano kuhusu jeshi la ulinzi la mkoa, kipengele kilicho muhimu katika mamlaka mpya ya UNMISS.
Vile vile leo, wajumbe hao wametembelea eneo la Wau, katika kituo cha ulinzi wa raia lililo karibu na kituo cha Umoja wa Mataifa cha Wau, pamoja na kanisa la kikatoliki lenye kuhifadhi wakimbizi wa ndani.
image