Ukosefu wa maji Tanzania bado ni mwiba kwa watoto wa kike- UNICEF

31 Agosti 2016

Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa limesema ingawa hatua zimepigwa katika kufikisha huduma ya maji safi na salama kwa baadhi ya maeneo nchini Tanzania, bado hatua zaidi zinahitajika ili kukwamua adha ya ukosefu wa maji kwa wanawake na watoto wa kike.

Mtaalamu wa mipango ya maji wa UNICEF nchini Tanzania Rebecca Budimu akihojiwa na Idhaa hii wakati huu ambapo dunia inaangazia wiki ya maji ametaja baadhi ya adha wapatazo watoto wa kike kutokana na ukosefu wa maji.

(Sauti ya Rebecca)

Amesema wakati serikali inachukua hatua kuhakikisha huduma ya maji inafikia wananchi kwa mujibu wa malengo endelevu, SDGs, jamii na sekta binafsi wana jukumu hivyo..

(Sauti ya Rebecca)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter