Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kulegeza msimamo kwa kila upande ndio suluhu Myanmar- Ban

Kulegeza msimamo kwa kila upande ndio suluhu Myanmar- Ban

Kufanyika kwa mkutano wenye lengo la kusaka suluhu ya mzozo wa kikabila nchini Myanmar ni hatua kubwa ya kihistori ambayo inapaswa kupigiwa chepuo, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika mkutano huo unaofanyika kwenye mji mkuu Nay Pyi Taw. Amina Hassan na ripoti kamili.

(Taarifa ya Amina)

Mkutano huo uitwao wa karne ya 21 wa Panglong unafanyika kusaka demokrasia katika nchi hiyo ya Myanmar iliyokuwa imegubikwa na mzozazo hadi uchaguzi wa wazi uliofanyika mwaka jana.

Ban amesema japo safari bado bado anapongeza nchi hiyo kwa hatua iliyofikiwa, sambamba na uvumilivu hasa kuleta pande zote kwenye meza moja kwa lengo moja ambalo ni mshikamano na amani, hivyo amesema..

“Nawasihi nyote kukubali kuwa hakuna pande inayoshiriki mchakato huu wa maridhiano unaweza kutarajia kukidhi malengo yake yote. Vivyo hivyo, kila upande ni lazima unufaike na kitu ili mchakato ufanikiwe. Utashi huu unataka nia njema kutoka kila upande na kutambua kuwa mafanikio hayo ni muhimu kwa maslahi ya wananchi wa Myanmar bila kujali kabila, dini, mrengo wa kisiasa au hadhi ya kiuchumi na kijamii.”