Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jitihada za amani Lebanon zaridhisha: Meja Beary

Jitihada za amani Lebanon zaridhisha: Meja Beary

Wakati Baraza la Usalama baadaye leo likitarajiwa kuwa na mashauriano kuhusu ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon UNFIL, Mkuu wa ujumbe huo ambaye pia ni mkuu wa vikosi vya UNFIL Meja Jenerali Michael Beary amesema hali ya usalama nchini humo imeimarika.

Katika mahojiano na redio ya Umoja wa Mataifa Jenerali Beary amesema licha ya changamoto ya machafuko nchini humo na ukanda mziama, jitihada za maridhiano na suluhu zinaridhisha.

Mteule huyo wa hivi karibuni ametaja yale atakayoyapa umuhimu katika uongozi wake.

( SAUTI BEARY)

‘‘Kipaumbele kikuu kwangu sasa ni kuhakikisha mgogoro hauibuki kwasababu yoyote ile na kutoka upande wowote. Kadhalika kuhakikisha tunaimarisha uwezo wa vikosi vya Lebanon.’’