Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya Aleppo Syria inasikitisha na zaidi kwa watoto:Lake

Hali ya Aleppo Syria inasikitisha na zaidi kwa watoto:Lake

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF , amesema ni binadamu gani anaweza kuona mateso ya Omran Dagneesh, kijana mdogo aliyeokolewa kutoka jengo lililoharibiwa huko Aleppo, Syria bila kusikitishwa?, akihoji pia, si watu wote wanapaswa kusikitishwa na zaidi ya watoto takriban laki moja ambao wamekwama Aleppo?.

Katika tamko lake maalumu, amesema haya yote ni maovu ambayo mtoto hapaswi kupitia na hata kuyaona. Hata hivyo amesema kusikitishwa na hasira haitoshi bali lazima iambatane na hatua za utekelezaji.

Akitoa mfano amesema watoto wa umri kama Omran huko Syria hawajui chochote ila ghasia na hofu za vita zinazoletwa na watu wazima. Hivyo akahimiza kuwa sote tunapaswa kuwadai hao watu wazima kuleta amani kwa  watoto wa Aleppo .