Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF:Mamia ya watoto waingizwa jeshini na makundi ya waasi Sudan Kusini

UNICEF:Mamia ya watoto waingizwa jeshini na makundi ya waasi Sudan Kusini

Tangu mwanzo wa mwaka huu watoto zaidi ya 650 wamesajiliwa na makundi yenye silaha nchini Sudan Kusini, limesema Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF.

Shirika hilo linasema kuna hofu kwamba mapigano mapya yanaweza kuwawaweka maelfu ya watoto katika hatari kubwa. Christophe Boulierac ni msemaji wa UNICEF..

(SAUTI YA CHRISTOPHE)

“Tunatoa wito wa kukomeshwa mara moja vitendo vya kuwaingiza watoto jeshini na kuwaachilia bila masharti watoto wote walio katika makundi yote yenye silaha.”

Inakadiriwa kuwa watoto 16,000 wamesajiliwa na makundi yenye silaha na majeshi na kulazimishwa kushiriki vita tangu kuzuka kwa machafuko Sudan Kusini Desemba 2013.