Skip to main content

WFP yakata msaada kwa wakimbizi, Uganda

WFP yakata msaada kwa wakimbizi, Uganda

Nchini Uganda, Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, limekata msaada wa pesa taslim na chakula kwa asilimia hamsini kwa wakimbizi, na kuzindua ombi la dola milioni ishriini ili kuziba pengo hilo hadi mwisho wa mwaka huu. John Kibego na maelezo zaidi.

(TAARIFA YA KIBEGO)

Katika taarifa ya pamoja ya WFP, serikali ya Ugand na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi , UNHCR, WFP, inahitaji msaada wa US$20million ili ianze tena kutoa msaada kwa 100% kwa takribani wakimbizi 200,000 waliowasili Uganda kabla ya July 2015, ambao wameathiriwa na mkato huu.

WFP imesema mkato huu unanza kutekelezwa wiki hii, lakini watu wenye mahitaji ya kipekee kama wazee na wasiojiweza hawataathirika, hata wawe miongoni mwa waliowasili Uganda kabla ya July 2015.

Mike Sackett, Mkurugenzi wa WFP, Uganda amesema, kufuatia ongezeko la wakimbizi kutoka sudan Kusini ambapo wakimbizi Zaidi ya 70,000 wameingia Uganda tangu July 8, hawakuwa na chaguo ila kukata msaada.

Ikiwa ni nyumbani kwa wakimbizi zaidi ya laki sita kwa sasa, Uganda ni nchi ta tatu kuhifadhi wakimbizi wengi zaidi barani Afrika, na ya nane duniani kote kulingana na report ya UNHCR ya mwaka 2015.