Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Apu ya WFP yatumiwa kuchangisha fedha kusaidia watoto Malawi

Apu ya WFP yatumiwa kuchangisha fedha kusaidia watoto Malawi

Kuanzia leo, Apu ya Shirika la Mpango wa Chakula (WFP) itatumiwa kuchangisha fedha za kusaidia jitihada za dharura nchini Malawi, kufuatia athari za makali ya hali ya hewa ya El Niño. Lengo la changisho hilo ni kuwezesha utoaji wa chakula kwa watoto wa shule 58,000 kwa mwaka mzima, katika wilaya ya Zomba kusini mwa Malawi, ambayo imeathiriwa sana na ukame na ambako sasa kuna uhaba mkubwa wa chakula.

Watoto hao wenye umri wa kati ya miaka Sita na miaka 13, watapewa uji wenye virutubishi, kupitia mpango wa WFP wa mlo shuleni. Utoaji wa mlo moto shuleni kila siku umedhihirika kuongeza idadi ya watoto wanaokwenda shule na kuboresha uwezo wao kusoma.