Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamati ya kutokomeza ubaguzi wa rangi yaanza kikao cha 90

Kamati ya kutokomeza ubaguzi wa rangi yaanza kikao cha 90

Kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu kutokomeza ubaguzi wa rangi, imefungua kikao chake cha 90 hii leo jijini Geneva, Uswisi, ikitarajiwa kutathmini juhudi za kupinga ubaguzi wa rangi nchini Ugiriki, Uingereza, Paraguay, Afrika Kusini, Lebanon, Ukraine, Sri Lanka na Pakistan.

Akifungua kikao hicho, Mkuu wa vikundi vinavyomulikwa katika Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Bwana Orest Nowosad, amesema licha ya kupitishwa mkataba wa kimataifa kuhusu utokomezaji wa aina zote za ubaguzi miongo mitano iliyopita, ulimwengu unashuhudia chuki, na ukatili tena katika baadhi ya jamii.

“Kwa kufuata nyayo za wanasiasa na viongozi, sauti za chuki na migawanyo zimeimerika, na baadhi ya watu wanajitenga kwa misingi ya “sisi” na “wao”. Kila siku tunashuhudia ukatili wa polisi kwa misingi ya rangi, na mauaji ya polisi kwa kujibu; na mawimbi ya uhalifu wa chuki dhidi ya vikundi vya walio wachache na unyanyasaji kwa misingi ya rangi, na ubaguzi na ukatili dhidi ya wahamiaji na wakimbizi unaongezeka. Visipodhibitiwa, kila kifo kinapanua pengo kati ya “sisi” na wao”