Haki za afya ya uzazi kwa wanawake Jamhuri ya Dominican (DR) ilindwe:UM

Haki za afya ya uzazi kwa wanawake Jamhuri ya Dominican (DR) ilindwe:UM

Kundi la wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa limewataka viongozi wa Jamhuri ya Dominican (DR) kulinda haki za wanawake na wasichana za kujamihiana na afya ya uzazi.

Wametoa wito kwa mamlaka kufuta kile wanachokiita “vizuizi” vya kisheria kuhusu suala la utoaji mimba. Bunge la seneti nchini humo linajadili mabadiliko kipengee cha sheria ambacho hakiharamishi fursa ya kutoa mimba katika mazingira haya matatu, mosi endapo afya na mama au msichana iko hatarini, pili kama mtu amebakwa au kuwa na uhususiano wa kingono na ndugu au mtu aliyeweza kuonana naye, na tatu endapo wamebaini mtoto hatoweza kuishi.

Mapendezo mapaya yanataka kuruhusu utoaji mimba katika hali moja tuu, ambapo afya ya mama au msichana ipo hatarini. Wataalamu wanasema kwa kufanya hivyo ni ukiukwaji mkubwa wa haki ya afya kwa wanawake na wasichana.